Mhudumu auwawa baada ya kuchelewesha huduma

Muktasari:

Taarifa iliyoripotiwa na AFP imeeleza wahudumu wa mgahawa huo waliita polisi baada ya kupigwa risasi begani mwenzao katika eneo la Noisy-le-Grand mashariki mwa Paris.

Paris. Muhudumu mmoja katika mgahawa jijini Paris amepigwa risasi hadi kufa na mteja ambaye amedaiwa kwamba alikuwa amekasirishwa baada ya kuagiza Sandwich ikacheleweshwa.

Taarifa iliyoripotiwa na AFP imeeleza wahudumu wa mgahawa huo waliita polisi baada ya kupigwa risasi begani mwenzao katika eneo la Noisy-le-Grand mashariki mwa Paris.

Wafanyakazi hao walijaribu kuokoa maisha ya muhudumu huyo ambaye alikuwa amepigwa risasi katika bega lake lakini alifariki papo hapo.

Wahudumu wenzake waliwaambia polisi kwamba mteja huyo alikuwa na hasira katika duka hilo la Pizza na Sandwich kutokana na muda mrefu ambao Sandwich hiyo ilichukua kuandaliwa.

Mshitakiwa wa mauaji alitoroka katika eneo la tukio na bado hajapatikana.

Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo, hatahivyo wamesema kwamba kumekuwa na ongezeko la visa vya uhalifu katika eneo hilo mbali na ongezeko la visa vya ulanguzi wa mihadarati pamoja na unywaji pombe barabarani