Mtoto wa Malkia akana kufahamu tabia chafu za rafikiye

Monday August 26 2019
pic princes

Mtoto wa malkia wa Uingereza, Prince Andrew amesisitiza kuwa "katika hatua yoyote ile" wakati wa urafiki wake na Jeffrey Epstein, ambaye alihukumiwa kwa kosa la biashara ya ngono kwa wasichana walio na umri dogo, alishuhudia "tabia yoyote ile ambayo ilisababisha mtu huyo akamatwe".
Andrew, mtoto wa pili wa kiume wa Malkia Elizabeth, amekuwa katika wakati mgumu kuhusu uhusiano wake na Epstein ambaye alikuwa akihusika na masuala yakifedha, na alikiri Jumamosi kuwa "ilikuwa makosa kumuona (Epsten) baada ya kuachiwa mwaka 2010".
"Katika wakati wowote ule wa uhusiano wetu uliokuwa na mipaka nikiwa naye sikuwahi kuona, kushuhudia au kushuku tabia ya aina ambayo baadaye ilisababisha akamatwe na kukutwa na hatia."
Epstein alikutwa akjiwa amekufa katika chumba chake gerezani mapema mwezi huu, na mtoto huyo wa Malkia aliwahi kuhusishwa naye baada ya video kutolewa ikijaribu kuonyesha kuwa alikuwa nyumbani kwa mhalifu huyo mwaka 2010.
Epstein alikiri kosa mwaka 2008 la kununua msichana aliye na umri chini ya miaka 18 aliyekuwa akifanya kazi ya kujiuza na alitumikia kifungo cha miezi 18 jela kabla ya kuachiwa kwa uangalizi.
"Nilifanya makosa kufikiri kwamba niliyemjua ndiye (Epstein) halisi, kw akuzingatia kile tunachokijua sasa," alisema Andrew.
"Huu ni wakati mgumu kwa kila mtu na sina uwezo wa kuelewa au kuelezea aina ya maisha ya Epstein," aliongeza.
Video hiyo ni mpya kati ya mambo kadhaa ambayo umekuwa yakichapishwa na magazeti kuweka bayana urafiki wa Prince Andrew na Epstein.
Gazeti la The Mail leo Jumatatu limesema mtoto huyo wa Malkia alimkaribisha Epstein katika nyumba ya Balmoral, ambayo ni makazi ya Malkia Elizabeth II nchini Scotland, mwaka 1999 katika muda ambao inawezekana malkia huyo alikuwa nyumbani.
Pia ameripotiwa kumkaribisha Epstein katika nyumba ya Sandringham, makazi ya kifalme yaliyoko mashariki mwa England, mwaka mmoja baadaye.
Epstein alifariki akiwa gerezani jijini Manhattan Agosti 10 wakati akisubiri kesi nyingine aliyoshtakiwa kwa shtaka moja la kusafirisha wasichana wenye umri madogo kwa ajili ya masuala ya ngono na kosa jingine la kufanya njama za kutenda kosa la usafirishaji wasichana wenye umri mdogo.
Epstein alijiua kw akujinyonga.
Kwa miaka kadhaa, Epstein alijiweka karibu na wanasiasa, watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii na wengine maarufu, akiwemo Donald Trump, kabla hajawa rais, na Bill Clinton.
Virginia Giuffre -- ambaye awali alikuwa akiitwa Virginia Roberts -- mmoja wa waathirika wa vitendo vinavyodaiwa kufanywa na Epstein, amesema alilazimishwa kufanya mapenzi na Prince Andrew jijini London wakati akiwa na umri wa miaka 17. Alisema alifanya naye tendo hilo la ndoa jijini New York na katika moja ya visiwa vya Carribea kinachomilikiwa na Epstein.
Lakini tuhuma hizo zilitupwa na Jaji wa Marekani mwaka 2015, aliyesema maelezo hayo hayakuwa yakitakiwa kuamua kesi ya madai inayomuhusu Epstein.

Advertisement