Mwana Mfalme apatikana na virusi vya Corona

Wednesday March 25 2020

 

By Mwandishi Wetu

London. Mwana Mfalme wa Uingereza Charles ambaye ndio Mrithi wa malkia Elizabeth amepatikana na virusi vya Corona, ofisi yake imesema leo Jumatano

Prince Charles ambaye ana umri wa miaka 71  yupo nchini Scotland na mke wake Camilla ambaye pia alipimwa  hakuonekana kuwa na virusi hivyo vya COVID-19.

Katika taarifa nyingine kutoka Buckingham Palace inasema malkia mwenye umri wa miaka 93, ana afya njema na hajaonana mwanae huyo kwa majuma mawili.

"Ni kweli, Prince Charles amepimwa na amepatikana na virusi hivyo. Amekuwa akionesha dalili  lakini ana afya njema  na amekuwa akifanya kazi kutokea nyumbani kwa siku kadha zilizopita,” taarifa hiyo ilisema.

Kulingana na maelekezo ya serikali  na ushauri wa kitabibu, Prince Charles na Mke wake wamelazimika kujitenga huko Scotland

Wanandoa hao walipimwa huko Aberdeenshire Kaskazini mashariki mwa Scotland, taarifa hiyo ilisema.

Advertisement

Advertisement