Mwandishi auawa, nyumba yake yachomwa moto

Monday November 4 2019

 

Kinshasa. Mtangazaji wa redio ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ameuawa nyumbani kwake katika eneo la Ituri, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa Jeshi la Congo, Jenerali Robert Yav akizungumza kutoka Mamabasa, Ituri, alisema washambuliaji wasiojulikana waliingia nyumbani kwa mtagazaji huyo, Papy Mahamba katika eneo la Lwemba na kumuua.
 Alisema kabla ya kutekeleza ukatili huo, walimjeruhi mke wake kabla ya kuchoma moto nyuma yao.
Mtangazaji huyo, anafahamika zaidi kwa kupambana na vita ya ugonjwa wa ebola.
Profesa Steve Ahuka, mratibu wa kitaifa wa mapambano dhidi ya ebola amethibitisha kuwa mfanyakazi mmoja aliyehusika katika vita dhidi ya ebola ameuawa katika eneo la Lwemba.
Mwanahabari katika kituo cha Radio Lwemba, ambako Mahamba alikuwa anafanya kazi pia amethibitisha maelezo hayo.
Jacques Kamwina ameliambia Shirika la habari la Ufaransa (AFP) kuwa Mahamba aliuawa nyumbani kwake kwa kuchomwa kisu.

Advertisement