Mwili wa Moi kuzikwa Februari 12

Wednesday February 5 2020

 

Nairobi. Mwili wa Rais mstaafu wa Kenya,  Daniel Arap Moi utazikwa nchini humo Jumatano ijayo Februari 12, 2020.

Taarifa iliyotolewa na familia yake Moi leo Jumatano Februari 5, 2020 imesema mazishi hayo yatafanyika nyumbani kwake Kabarak.

Mbunge wa Tiaty, William Kamket ambaye ni mjumbe wa kamati ya mazishi amesema mwili wake utaagwa katika uwanja wa mpira wa Kasarani, Jumanne Februari 11, 2020.

Moi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana Jumanne Januari 4, 2020 akiwa na umri wa miaka 95 katika Hospitali ya Nairobi alikokuwa anapata matibabu.

Advertisement