Papa Francis ameanza ziara Thailand na Japan

Wednesday November 20 2019

 

Thailand. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameanza ziara katika bara la Asia katika nchi za Thailand na Japan.

Ziara hiyo ya siku tatu ni ya kwanza kwa kiongozi huyo kutembelea katika nchi hizo.

Tayari kiongozi huyo amewasili mjini Bangkok, Thailand leo mchana Jumatano Novemba 20 ambako atakuwa na mazungumzo na mfalme Maha Vajiralongkorn na kiongozi wa jamii ya Wabudha nchini humo.

Jumamosi ijayo Papa Francis atakwenda nchini Japan anakotarajiwa kutoa ujumbe dhidi ya matumzii ya silaha za nyuklia kwenye miji ya Hiroshima na Nagasaki iliyoshambuliwa kwa mabomu wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.

Akiwa Japan, Papa Francis atakutana pia na manusura wa janga la kinu cha nyuklia cha Fukushima ambacho kiliharibiwa kutokana na tetemeko la ardhi na Tsunami mwaka 2011.

Papa Francis anakuwa kiongozi wa pili wa Kanisa Katoliki baada ya John Paul wa II kuyatembelea mataifa hayo ya barani Asia.

Advertisement

Advertisement