Papa Francis aonya chuki dhidi ya wageni

Wednesday September 11 2019

 

Vatican. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amesema chuki dhidi ya wageni barani Ulaya inayochochewa na siasa za kizalendo inakumbusha enzi ya Adolf Hitler katika miaka ya1930.

Kiongozi huyo wa kidini aliwaambia waandishi habari akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kumaliza ziara yake ya wiki moja barani Afrika alisema chuki dhidi ya wageni ni maradhi kama ya surua.

Papa Francis alisema kuwa maradhi hayo yanatumiwa kama sababu ya kujihami dhidi ya wageni wanaoonekana kuchafua damu ya taifa fulani.

Kiongozi huyo wa wakatoliki alisema tatizo hilo lipo hasa katika bara la Ulaya Afrika.

Kutokana na hali hiyo, Papa Francis ametoa wito kwa bara la Ulaya kujifunza kutokana na historia ya karne ya 20.

Advertisement