Rais Trump abadili timu yake ya mawasiliano

Washington, Marekani. Rais wa Marekani, Donald Trump amefanya mabadiliko katika kikosi chake cha mawasiliano katika Ikulu ya White House.

Katika mabadiliko hayo Stephanie Grisham ambaye alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano ameondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Kayleigh McEnany.

Grisham kwa sasa amepelekwa katika ofisi ya mke wa kiongozi huyo, Melania Trump.

Hata hivyo, Grisham aliyehudumu madaraka hayo kwa miezi tisa pekee hajawahi kufanya mkutano wowote na waandishi wa habari tangu kuteuliwa kwake.

Mabadiliko hayo yanajiri wakati nchi hiyo ikiwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Codiv-19 ambako zaidi ya watu 12,000 walifariki dunia.

Katika mabadiliko hayo Rais Trump pia alitangaza kuongeza idadi ya wafanyakazi wapya kwenye wizara ya mawasiliano na habari.

Kiongozi huyo alisema mabadiliko hayo yana lenga mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Ofisa wa ngazi za juu ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema msemaji wa makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon, Alyssa Farah atachukuwa majukumu mapya kama mkuu wa mawasiliano maalum ya kimkakati.

Farah ana mahusiano ya karibu kwa ikulu ya White House aliwahi kufanyakazi kama mkuu wa habari wa Mike Pence na mkurugenzi wa mawasilianao katika ofisi ya Meadow.