Rais Zuma kukata rufaa dhidi ya kesi yake ya ufisadi

Muktasari:

Rais Jacob Zuma amefikishwa mahakamani na kukabiliwa na mashtaka ya ufisadi, udanganyifu na utapeli wa fedha unaodaiwa kufanya katika miaka ya 1990.  Hata hivyo, Zuma amekana kuhusika na tuhuma hizo.

Johannesburg. Afrika Kusini. Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amewasilisha kusudio la kukata rufaa katika kesi yake ya ufisadi kupinga amri ya Mahakama Kuu iliyomtaka afike kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Wiki iliyopita Mahakama Kuu iliyopo KwaZulu-Natal, Afrika Kusini ilitupilia mbali utetezi wa Zuma uliokuwa ukipinga asifikishwe mahakamani na badala yake kumuru kiongozi huyo akufika kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Hata hivyo, wakati mahakama hiyo ikisubiri kufika kwa kiongozi huyo jana badala yake wakili wake, Thabani Masuku aliieleza mahakama kuwa mteja wake anakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Rais huyo wa zamani amefikishwa mahakamani na kukabiliwa na mashtaka ya ufisadi, udanganyifu na utapeli wa fedha unaodaiwa kufanya katika miaka ya 1990.  Hata hivyo, Zuma amekana kuhusika na tuhuma hizo.

 

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Zuma alipokea hongo ili kuhakikisha kampuni ya silaha ya Ufaransa Thales inapata zabuni.