Serikali yadhibiti ngono Siku ya Wapendanao

Muktasari:

  • Wananchi wa Indonesia wamejikuta wakisherehekea siku ya wapendano katika mazingira magumu baada ya polisi kuvamia hoteli, nyumba za kulala wageni na kudhibiti maduka ya kuuza condom wakitaka masuala ya ngono yafanywe na waliooana tu.

Indonesia haijapata ile hisia ya Siku ya Wapendanao leo kutokana na mamlaka kukamata wapenzi katika jiji moja, kuonya maduka yanayoonyesha condom na kuonya wanafunzi kuwa watakamatwa kama watajihusisha na vitendo vya mapenzi.
Makassar ambayo iko katika kisiwa cha Sulawesi  ilichukua hatua kali dhidi ya wakazi kwa kuvamia hoteli na nyumba za wageni jana na kukamata zaidi ya watu 20 ambao hawajaoa wala kuolewa, akiwemo Mjerumani mmoja.
"Tulimkamata Mjerumani na mpenzi wake katika hoteli na hawakuwa mume na mke ndio maana tuliwakamata," Iman Hud, kiongozi wa polisi aliiambia AFP.
Wapenzi hao wasiokuwa na bahati waliachiwa muda mfupi baadaye baada ya kupewa somo kuhusu ubaya wa kufanya mapenzi kabla ya ndoa, lakini watu watano wanaofanya biashara ya kuuza mwili watapelekwa katika kituo cha kurekebisha tabia, aliongeza.
"Huu ugonjwa wa kijamii lazima uzuiwe. Tunahitaji kuukumbusha umma kuendeleza utamaduni wetu na maadili," alisema Hud.
Siku ya Wapendanao ni tata kwa baadhi ya maeneo katika taifa hilo ambalo ni la Kiislamu, huku maimamu wengi na Waindonesia mahafidhina wakikosoa mizizi ya Kimagharibi na wanaizungumzia siku hiyo kama ya kuendeleza ngono kabla ya ndoa.
Lakini bado, wengine wengi wana uumini wa kati na wanasherehekea siku hiyo kwa kula chokleti na kupeana maua.
Mjini Makassar, hata hivyo, mamlaka zilikuwa zikikagua kutakakuona kama maduka yametii onyo lililotolewa awali la kutouza condom waziwazi na kukagua vitambulisho ili kung'amua kama wanunuaji si walio na umri mdogo.
"Condom ni kwa ajili ya watu wazima waliooana," alisema Hud.
"(Condom) hazitakiwi kuonyeshwa wala kuuzwa waziwazi, hasa karibu na sehemu wanazouza vyakula kwa watoto kama chokleti."