Trump amtimua mshauri wa usalama

Muktasari:

  • Ni John Bolton aliyekuwa akifanya kazi katika Ikulu ya Rais Donald Trump.

Washington, Marekani. Wakati Rais wa Marekeni, Donald Trump akitangaza kumfukuza kazi Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa nchi hiyo mwenyewe amedai kuwa amejiuzulu.

Kuondoka kwa John Bolton ambaye ndiyo msahauri mkuu wa kiusalama wa Ikulu ya Marekeni kumezua sitofahamu na kusababisha mjadala katika mitandao ya kijamii.

Jana Jumanne Septemba 10, Rais Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika kuwa "nilimjulisha John Bolton jana usiku kuwa huduma zake hazihitaji tena katika Ikulu ya White House.

 "Sikukubaliana sana na maoni yake mengi, kama walivyofanya wengine kwenye utawala na kwa hivyo, nilimuuliza John kwa kujiuzulu kwake, ambako nilipewa asubuhi ya leo. Namshukuru sana John kwa huduma yake. Nitamtaja mshauri mpya wa usalama wa kitaifa wiki ijayo,” alisisitiza Rais Trump.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kiongozi huyo wa Marekani kuandika hayo, Bolton alijitokeza na kutangaza kuwa ameamua kujiuzulu mwenyewe.

Bolton, mtaalam anayejulikana kwa maoni yake alikuwa mtu muhimu katika tawala za Marekeni.

Wakati huo huo, Urusi imesema kuwa kutimuliwa kwa Bolton hakutasaidia uhusiano na Marekani na kwamba uhusiano wake na nchi hiyo hautabadilika haraka.

Shirika la habari la Urusi (RIA), limemnukuu naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Rybkov akisema mara kwa mara Marekeni imekuwa ikifanya mabadiliko lakini hayaweki njia ya kuelekea katika kusawazisha uhusiano na nchi zingine.