UN: Hivi ndiyo wanachama wa Al-Shabaab wanavyojiunga

Muktasari:

Umoja wa Mataifa (UN) umetoa ripoti ya shambulio la kigaidi lililofanywa na kundi hilo katika Hoteli ya Dusit, Nairobi Kenya na kuua zaidi ya watu 26.

Nairobi, Kenya. Wakati maumivu ya vitendo vya kigaidi hayajapungua nchini Kenya Umoja wa Mataifa (UN) umetoa ripoti ya moja ya shambulio lilofanywa na kundi la Al-Shabaab.

Shambulio hilo lililotokea mwezi Januari katika Hoteli ya Dusit, Kenya na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 26.

Ripoti hiyo iliyotolewa Jumanne iliyopita Novemba 12, imeonyesha jinsi wafuasi wa kundi la Al-Shabaab wanavyopatikana na kuajiliwa nchini humo.

Ripoti hiyo ya wataalamu wa Umoja huo, pamoja na mambo mengine  imetaja Msikiti wa Musa uliopo mjini  Mombasa kuhusika katika kuwapa mafunzo wanachama hao.

Aidha, ripoti hiyo imewataja Wakenya watatu pamoja na Wasomali wawili kuwa ndiyo wafadhili wakuu wa kundi hilo ambako katika tukio hilo waliweza kuwaweka washambuliaji katika kambi ya Dadaab iliyopo Kaskazini Mashariki mwa Kaunti ya Garissa.

Shambulio hilo la kigaidi lililofanywa mwezi Januari mwaka huu linadaiwa kutekelezwa na kundi la  Al-Shabaab kwenye uwanja wa Hoteli ya Dusit iliyopo jijini Nairobi na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 26.

“Raia wa Kenya anayeishi Kaunti ya Mandera alikuwa kiungo muhimu wa ufadhili kati ya Al-Shabaab nchini Somalia na kiini cha kushambulia Kenya,” ilisisitiza ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kundi hili limeajiri ‘jeshi la wapiganaji’ kutoka kwa raia wenyewe wa Kenya.

Ilisema kuwa wanachama wa kundi hilo wana baraka za kiitikadi au ushirika na misikiti au mitandao ya kidini yanayopatikana nchini humo ikiongozwa na uongozi wa msikiti huo.

Ripoti hiyo pia ilimtaja Ali Salim Gichunge aliyezaliwa Isiolo mwaka 1995 kuwa ndiye mratibu mkuu wa shambulio hilo la Dusit lilosababisha watu 26 kupoteza maisha pamoja na mtu aliyejitoa muhanga kwa kujipiga risasi.

Ripoti hiyo ilimtaja raia huyo wa Kenya kwamba ndiye aliyepanga njama ili kufanikishha tukio hilo  na kusimamia moja kwa moja utekelezaji wake akiwa nchini Somalia.

Ripoti hiyo iligundua kuwa Gichunge na mkewe, Violet Wanjiru walipanga nyumba  katika jengo la Guango, Muchatha lililopo nje kidogo ya jiji la Nairobi miezi tisa kabla ya shambulio hilo ili kufanikisha mpango huo.

“Mkenya mwingine aliyejuliaka kwa jina la Osman Ibrahim Gedi, alikuwa mhudumu wa Gichunge alikuwa akisaidiana katika mipango hiyo na Siyat Omar Abdi, Msomali aliyezaliwa katika eneo la Dadaab, alikuwa mmoja wa watu wenye bunduki walioshambulia.