Umoja wa Mataifa kugawa chakula kwa waathirka wa mafuriko Kenya

Sunday November 10 2019

Nairobi, Kenya. Maelfu ya watu ambao waliokumbwa na uhaba wa chakula na kukosekana kwa huduma muhimu nchini Kenya watanza kupokea msaada wa chakula.

Wananchi hao wamekosa huduma muhimu baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyoharibu makazi yao.

Kwa mujibu wa Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP), shirika hilo linaisadia Serikali ya Kenya kuwasilisha chakula kwa familia kadhaa katika eneo la Kaskazini na Mashariki mwa kaunti za Mandera, Wajir, Garissa na Tana River.

Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa yalivunja madaraja na kuharibu barabara.

Taarifa ya Serikali ya Kenya ilisema kuwa tangu mwenzi Oktoba watu 38 wamefariki dunia na familia 11,700 zimepoteza makazi kutokana na mafuriko hayo.

Taaifa hiyo iliongeza kuwa zaidi ya wanyama 10,000 pia walikufa ambako Kitengo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha Kenya kimeonya kuwa mvua inaweza kuongezeka zaidi katika mwezi huu.

Advertisement

Advertisement