Urusi yaionya Marekani

Monday December 9 2019

Urusi. Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameionya Marekani kuhusu mpango wake wa upanuzi wa jeshi la anga.

Kwa muda mrefu mataifa yenye uwezo yakiwamo Urusi, China na Marekani yamekuwa yakitumia anga kwa manufaa yao kijeshi.

Akizungumza leo Jumatatu Desemba 9, Rais Putin alisema kwa sasa Marekani inaimarisha jeshi lake la anga kwa kasi ili kujiandaa kwa lolote lakini nchi yake haiitaji hilo.

“Kinachofanywa na Marekani lazima Urusi iwe na jibu lake, hatuwezi kunyamaza,” alisisitiza kiongozi huyo.

Rais Putin aliyekuwa akizungumza katika mkutano na maafisa wa ulinzi wa nchi hiyo alisema upanuzi wa jeshi la anga la Marekani ni tishio kwa maslahi ya Urusi.

Agosti mwaka huu, Rais Donald Trump alizindua kitengo kipya cha ulinzi chenye lengo la kulinda Taifa hilo na vita ya anga.

Advertisement

Kwa zaidi ya miaka 60 nchi za Marekani, Urusi na China zimekuwa zikijaribu silaha zao zinazoweza kuharibu setlaiti na kutumika kijeshi.

Advertisement