Vurugu zatawala mji wa Kivu

Tuesday November 26 2019

Hili ni kufuatia mauaji ya watu wanane yaliyofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kundi la waasi la ADF.

Kinshasa. Wananchi wenye hasira wamechoma moto ukumbi wa Jiji kwenye mji wenye ghasia wa Beni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Jambo hilo limetokea kutokana na mauaji ya watu wanane yaliyofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la waasi la ADF.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, msemaji wa jeshi la DRC,  Kanali Mak Hazukai amethibitisha mauaji hayo yaliyotokea karibu na mpaka wa DRC na Uganda.

Kamanda huyo amesema washambuliaji waliingia kwenye ukumbi wa Boikena na kuuwa raia hao.

Baada ya kuwasha moto huo, mwandishi wa AFP aliyeshuhudia tukio hilo, amesema watu waliandamana wakielekea kwenye kambi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa (Munusco) iliyoko nje kidogo ya Beni.

Advertisement

Kumekuwa na maandamano katika siku za karibuni dhidi ya walinda amani mjini Beni wanaolaumiwa kushindwa kuzuia mashambulizi ya mara kwa mara yanayodaiwa kufanywa na kundi la wapiganaji la Allied Democratic Forces (ADF).

Advertisement