Wagonjwa wa corona Kenya wafikia 31

Thursday March 26 2020

 

Nairobi, Kenya. Kenya imeripoti wagonjwa wapya watatu wenye maambukizi ya virusi vya corona na sasa wamefikia 31

Akitoa taarifa ya maambukizi ya ugonjwa huo, Katibu wa Waziri wa Afya nchini Kenya, Mercy Mwangangi amesema wagonjwa hao wapya ni raia wa Kenya ambao walikuwa karibu na wagonjwa walioripotiwa siku zilizopita.

Dk Mwangangi amesema kuwa watu wengine 906 waliokutana na wagonjwa hao wanafuatiliwa.

Kenye haijaripoti kifo chochote kinachotokana na virusi vya corona tangu kutangaza mgonjwa wa kwanza Machi 13, 2020.

Advertisement