Wagonjwa wa corona waongezeka Kenya

Muktasari:

Wizari ya Afya ya Kenya imethibitisha kuwapo kwa wagonjwa wapya watano wenye maambukizi ya virusi vya corona na kufanya idadi ya wagonjwa hiyo kufikia 184.

Nairobi. Kenya imeripoti wagonjwa wapya watano wenye maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Idadi hiyo mpya iliyotangazwa na Waziri wa Afya Kenya, Mutahi Kagwe leo Alhamisi Aprili 9, inafanya wagonjwa walioambukizwa virsi hivyo sasa kufikia 184.

Waziri Kagwe alisema kati ya wagonjwa hao wapya, watatu ni raia wa Kenya na wawili ni wa kigeni.

Alisema wagonjwa watatu wamegundulika jijini Nairobi na wengine walipatikana katika pwani ya Mombasa.

Katika hatua nyingine, mtu mmoja amefariki dunia kutokana na virusi hivyo mjini Mombasa na kufanya idadi ya waliopoteza maisha .saba hadi sasa ufikia saba.

Waziri Kagwe alisema tayari watu 12 wameripotiwa kupona ugonjwa huo na kuruhusiwa kurejea nyumbani.