Wamarekani watofautiana mauaji ya jenerali wa Iran

Muktasari:

  • Wabunge wa Democratic wanapinga kitendo hicho wakisema kitaibua mzozo Mashariki ya kati ambao Marekani na dunia hawawezi kuuvumilia.

Wabunge wa Republican wamesifu uamuzi wa Rais Donald Trump kufanya mashambulizi yaliyomuua mkuu wa kikosi cha kimapinduzi cha Iran, Qasem Soleimani, huku Bunge likilalamikia kuwa halikupewa taarifa zozote kabla ya shambulio hilo.

Pongezi hizo zinatofautiana sana na msimamo wa wabunge wa Democratic, ambao walikosoa vikali vitendo vay karibuni vya Trump wanavyoona ni vya kujijengea mazingira kabla ya uchaguzi wa rais.

"Katika kuonyesha kutatua tatizo na nguvu yetu, tulimpiga kiongozi wa wale wanaoshambulia maeneo huru ya Marekani," alisema Kevin McCarthy, mbunge wa Republica.

Kauli yake ilifanana na ya wabunge wengine wa Republicans.

"Wow - zawadi ya kuua na kujeruhi Wamarekani imepanda kwa haraka," alisema senata Lindsey Graham, mshirika wa karibu wa Trump, akiandika katika akaunti ya Twitter.

Shmabulio dhidi ya Soleimani, ambalo mlilitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad leo asubuhi nchini Iraq, pia lilimuua naibu kiongozi wa kundi la Hashed al-Shaabi, ambalo ni la wanamgambo.

Limekuja baada ya watu wanaoiunga mkono Iran kuvamia ubalozi wa Marekani kupinga kitendo cha taifa hilo kubwa duniani kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya kikundi hicho.

Marekani iliamua kufanya mashambulizi kujibu shambulio la makombora ya roketi yaliyofanywa siku chache kabla na ambayo yalimuua mkandarasi wa Marekani aliyekuwa akifanya kazi nchini Iraq.

Kwa kawaida ikulu ya Marekani, inayijulikana zaidi kama White House, hutoa taarifa kwa wabunge waandamizi wa vyama vyote katika chombo cha Seneti na wawakilishi kabla ya shambulio lolote kubwa la kijeshi.

Lakini mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Eliot Engel alisema katika taarifa yake kuwa shambulio "lilifanyika bila ya taarifa au mashauriano na Bunge."

Soleimani alikuwa "mbunifu mkuu wa vurugu kubwa" na ambaye "ana damu za Wamarekani mikononi mwake," mbunge huyo wa Democratic alisema.

Lakini "kuendelea na kitendo cha ukubwa huu bila ya kulitaarifu Bunge ni tatizo kubwa kisheria na ni kudharau nguvu za Bunge kama sehemu ya serikali," alisema Engel.

Hali kwa upande wa Democratic ilikuwa ya kupinga vikali shambulio hilo, huku spika wa Bunge, Nancy Pelosi akisema kumuua kiongozi wa juu ya kijeshi kunachokoza kuongezeka kwa vurugu.

"Marekani-- na dunia-- haiwezi kuvumilia hali hii ya wasiwasi kuendelea hadi kufikia sehemu isiyovumilika," alisema katika taarifa yake.

Wagombea urais katika kampeni za mwaka 2020 pia walikuwa wakipima suasa hilo.

Joe Bidden, ambaye anaongoza kundi la wagombea urais kutoka Democratic, alisema Rais Trump amewasha moto.

"Hakuna shaka Iran italipiza kisasi. Tunaweza kuwa mwanzoni mwa mzozo mkubwa Mashariki ya Kati," alisema Biden.