Wanafunzi 27 wafariki dunia kwa moto Liberia

Wednesday September 18 2019

Monrovia, Liberia. Wanafunzi 27 wa shule ya kiislamu wamefariki dunia nchini Liberia kwa kuungua moto ulioteketeza bweni la shule hiyo iliyopo mjini Monrovia.

Moto huo ulitokea jana asubuhi Jumanne Septemba 18 wakati mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo alipokuwa amelala katika moja ya bweni hilo lilipo karibu na msikiti.

Polisi nchini humo walidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuliambia Shirika la habari la BBC kuwa bado wanaendelea kutoa maiti katika jengo hilo kutokana na wengi wao kuungua vibaya.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, wanafunzi walioathirika na moto huo ni kati ya umri wa miaka 10 na kuendelea.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Liberia George Weah alitoa salamu zake za rambirambi na kuwapa pole familia ya wanafunzi hao.

Taarifa ya msemaji wa Rais kwa vyombo vya habari ilisema kuwa Rais Weah amepanga kuhudhuria mazishi ya wanafunzi hao ambayo yamepangwa kufanyika leo Jumatano.

Advertisement

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Liberia, Moses Carter alilimbia Shirika la habari la Reuters kwamba ingawa uchunguzi unaendelea lakini taariza za awali zinasema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.

Mchungaji Emmanuel Herbert ambaye alishughudia tukio hilo aliiambia BBC alisikia sauti ya wanafunzi hao wakilalamika moto na ghafla alisikia king’ora kinachoashiria kuwapo kwa hatari ya moto katika neo hilo.

"Nilipoangalia kupitia dirishani, niliona eneo zima limefunikwa na moto,” alisisitiza mchungaji Herbert.

Hata hivyo, mchungaji huyo alisema hakuweza kuingia katika eneo hilo kwa kuwa jengo hilo lilikuwa na mlango mmoja pekee  ambao ulifungwa.

T. Wanafunzi 27 wafariki dunia kwa moto Liberia

S. Ni baada ya bweni lao kuwaka moto na kuteketea kabisa huku wengi ni wa umri wa miaka 10 na kuendelea.