Wanawake wapungua matumizi ya mtandao duniani

Muktasari:

  • Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Mawasiliano dunia (ITU) inaonyesha kuwa watumiaji wa mtandao wa internet wameongezeka lakini wanawake wakipungua.

Geneva Uswizi, Ripoti mpya ya Shirika la Kimataifa la Mawasiliano duniani (ITU) inaonyesha kuwa idadi ya watu wanaotumia mtandao wa intaneti imeongezeka kwa karibu mara nne zaidi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi hiyo sasa imefikia bilioni 4.1 tangu mwaka 2005.

Hata hivyo, licha ya ongezeko hilo, idadi ya wanawake wanaotumia intaneti imeshuka kwenye maeneo kadhaa.

Ripoti hiyo imeonya kuwa pengo kati ya wanaume na wanawake wanaotumia mtandao limeongezeka barani Afrika kwenye nchi za Kiarabu, eneo la Asia na Pasifiki.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana Jumanne Novemva 5 mjini Geneva, Uswizi inasema kwamba matumizi ya mtandao wa intaneti yameongezeka ulimwenguni kwa asilimia 54.

“Bado watu bilioni 3.6 hawatumii mtandao huo hasa kwenye nchi zinazoendelea,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.

ITU imetaka hatua zichukuliwe katika kuongeza umiliki wa simu za mkononi miongoni mwa wanawake na kuanzisha ujuzi wa msingi wa kidijitali kwenye nchi zinazoendelea duniani.