Watu wanne wapigwa risasi wakiangalia mpira California

Muktasari:

Inaelezwa kuwa watu wote waliouawa pamoja na majeruhi sita ni wanaume wenye umri kati ya miaka 25 na 35.

Los Angeles, Watu wanne wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi wakati wakiangalia mpira.

Polisi mjini California wamesema kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita wakati watu hao wakitazama mpira katika eneo la wazi lililopo

Kwa mujibu wa jeshi hilo, polisi waliitwa katika tukio baada ya mtu mmoja kufyatua risasi za moto katika mkusanyiko wa zaidi ya watu 35 waliokuwa katika nyumba iliyopo eneo la Fresno, kilometa 320 Kaskazini mwa mji wa Los Angeles.

“Watu watatau walifariki dunia katika eneo la tukio,” naibu kamishana wa polisi wa eneo la Fresno, Michael Reed aliwaambia waandishi wa habari.

Kamanda huyo alisema mmoja kati ya majeruhi hao alifikishwa hospitalini lakini hata hivyo, alipoteza maisha muda mfupi bada ya kufikishwa kutokana na majereha makubwa aliyoyapata.

Kamanda Reed alisema watu wote wanne waliouawa pamoja na majeruhi sita ni wanaume wenye umri kati ya miaka 25 na 35.

“Tunazipa pole familia zote zilizopoteza wapendwa wao… tukio hili ni la kipumbavu na linapaswa kulaaniwa.

“Tunafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha waliohusika na tukio hili wanachukuliwa hatia kwa mjibu wa sheria.”

Hata hivyo, kamanda huyo alisema mpaka sasa hakuna taarifa rasmi juu ya waliohusika na tukio hilo na kwamba hakuna viashiria vinavyoonyesha kuhusika na tukio linalofanana na hilo,” alisema.

Msemaji wa polisi katika jimbo la California, Bill Dooley alisema kwa sasa Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi Ili kubaini waliohusika kwa kuhoji watu walioshuhudia tukio hilo.