Watu wawili wauawa kwa risasi Marekani

Muktasari:

 Tukio hilo lilitokea nje ya Chuo Kikuu cha kibiashara cha A&M kilichopo katika eneo la Greenville, umbali wa kilometa 24 Kusini Mashariki mwa jimbo la Texas.

Texas, Marekani. Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine 14 kujeruhiwa nje kidogo ya Chuo Kikuu cha kibiashara cha A&M jimboni Texas, Marekani.

Ofisa mwandamizi wa polisi, Buddy Oxford alisema kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Greenville, umbali wa kilometa 24 Kusini Mashariki mwa jimbo hilo.

Hata hivyo, afisa huyo alisema polisi inaendelea na uchunguzi ili kubaini aliyefanya uhalifu huo.

“Majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini. Mshambuliaji aliyehusika na tukio hilo bado anasakwa,” alisisitiza ofisa huyo.