Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akutwa na virusi vya corona

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amepimwa na kubainika kuwa na virusi vya corona, ofisi yake ya Downing Street imeeleza.
Johnson alichukuliwa vipimo vya ugonjwa huo ambao umeua zaidi ya watu elfu kumi duniani, baada ya kupata dalili kadhaa za ugonjwa wa corona.
"Nimekuwa na dalili ndogo za corona, ambazo ni viwango vya juu vya joto la mwili na kikohozi ambacho hakikomi," alisema Johnson katika video aliyoituma kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Twitter.
Hata hivyo, Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema kuwa ataendelea kulingoza taifa kutoka nyumbani licha ya kuwa na ugonjwa huo wa Covid-19.