Mwanyika atangazwa mshindi Jimbo la Njombe

Muktasari:

Uchaguzi huu ulifanyika jana Jumatano, Oktoba 28, nchi nzima.

Njombe. Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Njombe Mjini, Deo Mwanyika ametangazwa kuwa wa nafasi hiyo baada ya kuwashinda  Emmanuel Masonga wa Chadema na Edward Wiliam wa DP.

Akitangaza matokeo hayo asubuhi hii ya Alhamisi Oktoba 29, 2020, msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Njombe, Iluminata Mwenda aamesema Mwanyika ameshinda kwa kura 29,553 akifuatiwa na Emmanuel Masonga aliyepata kura 5,940 na Edward Wiliam wa DP aliyepata kura 162.

Jumla ya kura zilizopigwa jimboni humo ni 36,364 kutoka vituo 271.

Hata hivyo, idadi ya wananchi waliojitokeza jana kupiga kura ni ndogo ikilinganishwa na ya waliojiandikisha kupiga kura jimboni humo waliofikia 96,884.

Endelea kufuatilia mitandao yetu ya Mwananchi kwa matokeo zaidi