Breaking News

Romero kulazimisha kuondoka Man United

Friday October 16 2020

 

Manchester, England. Sergio Romero ameiomba Manchester United kumwacha aondoke baada ya kushindwa kuondoka wakati wa usajili wa dirisha kubwa lililofungwa wiki iliyopita.

Kipa huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye miaka 33, alikuwa akitamani kuondoka Old Trafford, wakati Everton walipokuwa katika mazungumzo na Man United.

Romero alishindwa kutamba mbele ya David De Gea na sasa amerudi Dean Henderson katika idadi ya makipa kutokana na kiwango bora alipokuwa kwa mkopo Sheffield United.

Mke wa kocha huyo pia alionekana kumtaka Ole Gunnar Solskjaer kumwachia mumewe akatafute maisha sehemu nyingine kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Taarifa zinadai kuwa Romero na mkewe walikasirika baada ya kugundua kuwa Everton ilikuwa tayari kulipa mshahara wa Pauani 100,000 kwa wiki kwa Romero.

Kipa huyo ameanza upya kwa sasa kutaka nafasi ya kuondoka Man United na inadaiwa ameomba mkataba wake kukatishwa ili kusaka maisha mapya ya kucheza sehemu nyingine.

Advertisement

Inaaminika kuwa kipa huyo aliyepoteza matumaini ya kucheza Old Trafford hataki hata malipo katika kusitisha mkataba wake, licha ya kulipwa Pauni 1.5 milioni kwa mwaka.

Advertisement