Yvone: Nilitumia siku tatu kufanya uamuzi wa kukubali mwanangu akatwe mkono - VIDEO

Siku 10 baada ya Yvone kujifungua mtoto wake alianza kuumwa hali iliyosababisha kurudishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ambako aliandikiwa dozi ya sindano 14.

Yvone alieleza kuwa matibabu hayo yatafanyika mtoto akiwa amelazwa na aliwekewa cannula (mrija unaotumika kupitishia dawa kwenye mshipa).

Siku ya tatu baada ya kuanza dozi, muuguzi alimuwekea dawa mtoto asubuhi lakini wakati akifanya hivyo mtoto alilia kupita kiasi.

Hali hiyo ikawapa wasiwasi wauguzi hao na kulazimika kuanza kumfanyia uchunguzi mtoto huyo lakini hawakuweza kubaini tatizo.

Alieleza kuwa ilipofika jioni ya siku hiyo, muuguzi wa zamu alimchunguza mtoto na kubaini kuwa vidole vyake viwili vimeanza kuwa vyeusi.

Alisema siku iliyofuata alipita daktari mwingine aliyemuona mtoto huyo na kushtushwa na hali aliyokuwa nayo na hatimaye akampa rufaa ya kwenda Muhimbili ambako alifanyiwa uchunguzi na ikaonekana ni lazima kiganja hicho kiondolewe.

Pata Simulizi hii katika gazeti la mwananchi la Septemba 11, 2019, pamoja na kutizama Video iliyoambatanishwa hapa