VIDEO: Serikali yawasilisha hoja nane pingamizi kesi ya mkulima anayehoji ukomo wa urais

Mkulima Patrick Dezydelius Mgoya 

Muktasari:

Serikali imemuwekea pingamizi mkulima Patrick Dezydelius Mgoya aliyefungua kesi ya kikatiba inayohoji ukomo wa kipindi cha urais wa Tanzania.


Serikali imemuwekea pingamizi mkulima Patrick Dezydelius Mgoya aliyefungua kesi ya kikatiba inayohoji ukomo wa kipindi cha urais wa Tanzania.

Mkulima huyo, mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam, amewekewa pingamizi la awali na Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayeiomba mahakama iitupilie mbali kesi hiyo bila hata kuisikiliza.

Pingamizi la Serikali lilibainishwa na wakili Daniel Nyakiha jana kesi hiyo ilipotajwa mara ya kwanza mahakamani tangu ilipofunguliwa mwezi uliopita.

Mkulima huyo amefungua kesi hiyo Mahakama Kuu dhidi ya AG, akiiomba mahakama itoe tafsiri sahihi ya ibara ya Katiba inayoweka ukomo huo wa urais.

Kesi hiyo ilitajwa mara ya kwanza jana mbele ya majaji watatu wanaoongozwa na Jaji Kiongozi, Dk Eliezer Felesh. Majaji wengine ni Dk Benhajj Masoud na Seif Kulita.

Hata hivyo wakili, Nyakiha aliieleza mahakama kuwa wamewasilisha majibu yao na pingamizi la awali lenye hoja nane.