Jesephta Mukobe: Mwanamke mlemavu aliyepambana sasa ni katibu mkuu wa Wizara

Kumekuwa na malalamiko ya watoto wenye ulemavu kufungiwa ndani kutokana na familia nyingi kuamini kuwa watoto hao wana nuksi badala ya baraka.

Watoto hao imewahi kutokea mara kadhaa kugunduliwa na majirani ambao hupiga kelele na hatua stahiki kuchukuliwa ikiwamo kuwapeleka hospitali na kupata tiba, ingawa kwa kuchelewa sana. Baadhi yao hupoteza maisha kutokana na kuchelewa kupata huduma.

“Pamoja na ulemavu niliozaliwa nao wazazi wangu hawakunichukulia kama nuksi kwenye familia, badala yake walinitanguliza mbele kuhakikisha ninatimiza ndoto zangu,”anaanza kusimulia Jesephta Mukobe.

Jesephta Mukobe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo, Utamaduni na Urithi, nchini Kenya, alikuwa hapa nchini kuhudhuria tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest) lililomalizika hivi karibuni.

Ushiriki wake na harakati za kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa kwa washiriki kutoka nchini mwake licha ya kuwa ni miongoni mwa watu wenye ulemavu, kulimvutia mwandishi wa makala haya kutaka kufahamu changamoto alizopitia na mafanikio yake.

“Miaka niliyozaliwa tofauti na sasa hali ilikuwa mbaya sana kwenye nchi za Afrika ikiwamo Kenya, ambapo mama akijifungua mtoto mwenye ulemavu kama mimi ilichukuliwa kuwa ni nuksi na hata kuuawa,” anasema Jesephta.

Anasema licha ya kuzaliwa mlemavu amefanya kazi serikalini kwa miaka 33 akihudumu kwenye wizara nne tofauti.

Kwa undani wa habari hii pata nakala ya Gazeti la Mwananchi, Jumapili Oktoba 13.