Chadema yatoa orodha wanaowania ujumbe kamati kuu

Muktasari:

Kamati kuu ya Chadema yaweka hadharani majina wa waliopitishwa kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati kuu wamo wabunge wa viti maalumu na majimbo wanaomba kuteuliwa.

Dar es Salaam. Kamati ya kuu ya Chadema nchini Tanzania iliyokutana leo Jumatatu Desemba 16, 2019 imepitisha majina mbalimbali ya wanachama wa chama waliomba nafasi ya ujumbe wa kamati hiyo.

Orodha hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Uenez, Mawasiliano  na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema wakati akitoa mrejesho kwa  wanahabari  kuhusu kikao cha kamati kuu kilichoketi.

Amewataja waliopitishwa na kamati kuu kwa upande wanaume ni Gibson Meiseyeki ambaye ni mbunge wa Arumeru Magharibi, Patrick Ole Sosopi, Samson Mwambene, Mechard Tiba na Ahobokile Mwaitenda.

Upande wa wanawake ni wabunge wa chama hicho, Suzani Kiwanga (Mlimba), Pamela Massay (Afrika Mashariki) na Grace Kiwelu (viti maalumu) na wengine ni Catherine Vermand, Ester Daffi, Sara Katanga na Betty Massanj.

"Upande wa kundi la wanawake watakaochaguliwa ni watatu vivyo hivyo kwa kundi la  wanaume. Idadi ya wajumbe wanaotakiwa kwa mujibu wa katiba ni wanane sita kutoka bara na wawili Zanzibar," amesema Mrema.

"Wajumbe wa kamati kuu wanaume kwa upande w Zanzibar waliopitishwa ni Hemed Ali Hemed na Yahya Alawi Omary. Upande wa wanawake ni Sharifa Suleiman Suleiman, Zeud Mvano Abdillah na Zainab Mussa Bakar.

Mrema amesema majina hayo yatapelekwa kwenye baraza kuu la chama hicho  litakaloketi Desemba 19, 2019 kwa ajili ya kufanya uteuzi wa majina nane.