VIDEO:Maisha ya Pius Msekwa nyumbani kwake Ukerewe

Maisha ya Pius Msekwa nyumbani kwake Ukerewe

Muktasari:

Haya ndio maisha ya Pius Msekwa baada ya kustaafu. Ndivyo unavyoweza kusema ukifika nyumbani kwa makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM-Bara, Pius Msekwa.

Dar es Salaam. Haya ndio maisha ya Pius Msekwa baada ya kustaafu. Ndivyo unavyoweza kusema ukifika nyumbani kwa makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM-Bara, Pius Msekwa.

Spika huyo wa zamani wa Bunge anaishi mtaa wa Nkilizya mjini Nansio wilayani Ukerewe.

Ukifika nyumbani kwake unaweza kushangaa uzuri wa bustani iliyoipa jina la Hifadhi ya Serengeti kwani imejaa sanamu za wanyama mbalimbali.

Pamoja na sanamu za wanyama, bustani hiyo  ina wanyamapori halisi waliokaushwa na mti wenye matawi yenye rangi ya kijani na njano inayotumiwa na CCM iliyowekewa ubao wenye maneno “Mti wenye majani yenye rangi za CCM”.

Bustani hiyo pia ina bwawa linalowakilisha Ziwa Victoria ikiwa na sanamu za mamba, miamba, milima na mitumbwi ya wavuvi, miti ya matunda na dawa, michoro ya aina za samaki wanaopatikana katika ziwa hilo  pamoja na utamaduni, mafunzo ya historia, mila na desturi za wenyeji wa Wilaya ya Ukerewe.