Wagombea ubunge wadai Magufuli atamaliza migogoro ya ardhi Manyara

Muktasari:

Wagombea ubunge wa majimbo ya Mkoa wa Manyara kupitia CCM wamedai kuwa mgombea urais wa chama hicho, John Magufuli akichaguliwa tena kwa kipindi cha miaka mitano atamaliza migogoro ya ardhi mkoani humo.

Babati. Wagombea ubunge wa majimbo ya Mkoa wa Manyara kupitia CCM wamedai kuwa mgombea urais wa chama hicho, John Magufuli akichaguliwa tena kwa kipindi cha miaka mitano atamaliza migogoro ya ardhi mkoani humo.

Mbunge mteule wa jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul akizungumza Oktoba 25 kwenye uwanja wa Kwaraa amesema mgombea urais Dk Magufuli atatatua migogoro ya ardhi iliyobaki.

"Migogoro mingi ya ardhi imemalizika kipindi cha miaka mitano ya Rais Magufuli, hivyo tumuongezee kipindi kingine cha miaka mitano ili migogoro miwili ya Dudumera na Tina imalizike," amesema Gekul.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema Dk Magufuli akichaguliwa tena kwa miaka mitano atatatua mgogoro wa wafugaji na pori la Mkungunero.

“Pia atatatua mgogoro wa mashamba makubwa na wananchi kwenye kata ya Simanjiro,” amesema Ole Sendeka.

Kwa upande wake, mgombea ubunge wa jimbo la Kiteto, Edward Ole Lekaita amesema migogoro mingi ya ardhi imemalizika kwenye eneo hilo ila bado migogoro ya mtu na mtu ambayo inaendelea kutatuliwa.

Mgombea ubunge wa jimbo la Hanang' mhandisi Samwel Hhayuma amesema akichaguliwa kushika nafasi hiyo atahakikisha dhana ya Tanzania ya viwanda inatekelezwa pia Wilayani Hanang'.

Babati. Wagombea ubunge wa majimbo ya Mkoa wa Manyara kupitia CCM wamedai kuwa mgombea urais wa chama hicho, John Magufuli akichaguliwa tena kwa kipindi cha miaka mitano atamaliza migodi ya ardhi mkoani humo.