Madiwani CCM washinda kata zote 20 jimbo la Arumeru Mashariki

Muktasari:

  • Matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambapo mgombea wa CCM John Pallangyo anachuana na mgombea wa Chadema Rebecca Mgodo yanatarajiwa kutangazwa muda wowote kuanzia sasa.

Àrusha. Wagombea wote wa udiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) katika kata 20 zilizofanya uchaguzi kati ya kata 26 jimbo la Arumeru Mashariki wameshinda.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo, Emmanueli Mkongo amesema katika jimbo hilo Kata Sitawagimbea wa CCM walipita bila kupingwa.

Amesema  Jimbo lilikuwa na vituo 521 vya kupiga kura na idadi ya wapiga kura walioandikishwa  jimboni humo ilikua 194,367.

Matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambapo mgombea wa CCM John Pallangyo anachuana na mgombea wa Chadema Rebecca Mgodo yanatarajiwa kutangazwa muda si mrefu.

Endelea kufuatilia mitandao yote ya Mwananchi kwa matokeo zaidi na chanya.