VIDEO: Afya ya Ruwa’ichi yaimarika, aanza kula

Wednesday September 11 2019

 

By Elizabeth Edward, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Afya ya Askofu mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam nchini Tanzania, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi aliyefanyiwa upasuaji wa dharura katika taasisi ya mifupa (Moi) imeimarika.

Ruwa’ichi alifanyiwa upasuaji wa kichwa jana Jumanne Septemba 10, 2019 katika taasisi hiyo kwa ajili ya kuondoa damu iliyoingia katika ubongo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Septemba 11, 2019 daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, Profesa Joseph Kahamba amesema afya yake imeimarika.

“Mhashamu anaendelea vizuri ameamka, anazungumza anajitambua na anakula mwenyewe halishwi kwa mipira wala hategemei mashine ya kumsaidia kupumua. Amepata nafuu haraka.”

“Tunamuangalia kwa ukaribu kwa sasa yupo ICU ila kadiri atakavyoendelea tutamhamishia katika wodi ya kawaida,” amesema.

Amesema akiendelea vyema watamruhusu kurejea nyumbani, kuendelea kumuangalia kama mgonjwa wa nje.

Advertisement

Amesema watakapoona anaendelea vyema watamruhusu kurejea nyumbani huku wakiendelea kumuangalia kama mgonjwa wa nje.

Advertisement