Ajali ya moto Morogoro ilivyorejesha machungu ya vifo vya wanakijiji mwaka 2000

Ojoku Lwijisi. Picha na Godfrey Kahango

Muktasari:

Miaka 19 iliyopita, Ojoku Lwijisi alinusurika katika ajali ya moto iliyochukua maisha ya mwenzake na wanakijiji wengine zaidi ya 40 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika Kata ya Isongole wilayani Rungwe

Mbeya. Miaka 19 iliyopita, Ojoku Lwijisi alinusurika katika ajali ya moto iliyochukua maisha ya mwenzake na wanakijiji wengine zaidi ya 40 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika Kata ya Isongole wilayani Rungwe.

Moto huo ulitokana na lori lililokuwa na shehena ya mafuta aina ya petroli, likitoka Dar es Salaam kwenda Malawi lakini likapinduka Idwele, kilomita chache kutoka Mbeya Mjini.

Leo hii mwili unamsisimka baada ya kumbukumbu za tukio hilo kumrejea kutokana na ajali kama hiyo kutokea Agosti 10, 2019 mjini Morogoro na kuchukua maisha ya watu 94 hadi jana mchana.

“Kila ninaposikia tukio hilo, moyo unakufa ganzi na kuanza kutokwa machozi,” anasema Lwijisi katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika Kijiji cha Idwele ambako lori hilo lilipinduka na baadaye kulipuka baada ya kijana mmoja kujaribu kuchomoa betri iliyosababisha cheche na mafuta kushika moto.

“Unajua bila kupepesa macho, ni tamaa yetu ndio ilituponza. Kwa mfano, tulifanikiwa kuchota mafuta, tukarudi tena kutaka kuchota mengine. Tulipoona yameisha, mwenzangu akaingiwa na tamaa nyingine na kwenda kuchomoa betri ili aondoke nayo na kilichotokea ndiyo hiki.”

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumapili Agosti 18, 2019