Ajax ilivyopukutishwa baada ya kung'ara Ulaya, inavyojijenga

Muktasari:

Ajax inajiandaa kuivaa Liverpool katika mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya itakayofanyika Jumatano, ikiwa imesukwa upya baada ya wachezaji waliong'ara mwaka 2019 kununuliwa na klabu tajiri

 

Amsterdam, Uholanzi (AFP). Ajax itakuwa mwenyeji wa Liverpool katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kesho Jumatano, ikiwa ni miezi 18 baada ya kukataliwa nafasi ya kucheza na klabu hiyo ya Anfield katika fainali kutokana na Tottenham Hotspur kuzinduka katika mechi ya nusu fainali jijini Amsterdam.

Klabu hiyo ya Udachi ililishangaza bara la Ulaya msimu huo hadi kufikia nusu fainali, kabla ya wachezaji wake kunaswa na klabu tajiri zaidi.

AFP Sport inaangalia kilichosalia katika timu ya Ajax:

 

- Beki wa bei kali -

Majina makubwa yaliyohama majira ya joto mwaka 2019 ni wachezaji wawili wa kimataifa wa Uholanzi Matthijs de Ligt na Frenkie de Jong.

Beki wa kati-back De Ligt, ambaye alikuwa nahodha wa Ajax mwaka huo akiwa na umri wa miaka 19, alifunga bao la ushindi dhidi ya Juventus katika mechi za robo fainali na pia akafunga dhidi ya Tottenham katika nusu fainali. Alihamia Juve kwa ada ya euro 75 milioni (sawa na dola 84.2 milioni) na euro 10.5 milioni juu, rekoi ya dunia kwa beki.

Wakati huo, kiungo De Jong, sasa ana miaka 23, aliuzwa kwenda Barcelona katika uhamisho uliogharimu euro 86 milioni uliokubaliwa katikati ya msimu wa mwkaa 2018-19.

Kasper Dolberg alikuwa sehemu ya timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa, lakini bado Ajax ikaingiza fedha kwa mshambuliaji huyo wa Denmark, aliponunuliwa kwa klabu ya Nice ya Ufaransa kwa euro 20.5 milioni. Mchezaji mwingine kutoka Denmark, kiungo mkongwe Lasse Schone, aliondoka kwenda Genoa ya Italia.

Baada ya kushindwa kuvuka hatua ya makundi msimu uliopita, Ajax iliruhusu wachezaji wengine kuondoka, wakati kiungo wa kimataifa wa Morocco mwenye talanta kubwa, Hakim Ziyech alipojiunga na Chelsea kwa euro 40 milioni.

Na Donny van de Beek ni mchezaji wa mwisho kuondoka. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 na ambaye alifunga bao pekee ugenini dhidi ya Spurs katika mechi ya kwanza ya nusu fainali, alinunuliwa na Manchester United mwezi Septemba kw aeuro 39 milioni.

Kwa ujumla, Ajax ambayo imetwaa ubingwa wa Ulaya mara nne, iliingiaza karibu euro 300 milioni kwa kuuza wachezaji waliokuwa katika kikosi hicho kilichofanya maajabu Ulaya na kilichotwaa mataji mawili ya nyumbani mwaka 2019.

 

- Waliosalia -

Wachezaji wengi vijana waliong'ara katika kikosi hicho wameondoka, lakini wengine wamesalia. Erik ten Hag bado ni kocha, wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Serbia, Dusan Tadic bado ni tegemeo la Ajax kw amabao.

Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton alifunga mabao sita katika kampeni hiyo ya Ajax Ulaya na alifunga mabao 16 msimu uliopita ambao ulifupishwa kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, na kuisha bila ya bingw akutangazwa. Tadic pia alifunga mabao mawili mwishoni mwa wiki wakati Ajax iolipoizamisha Heerenveen kwa mabao 5-1.

Kipa Andre Onana, beki wa kati Daley Blind, beki wa kushoto Muargentina Nicolas Tagliafico na beki wa pembeni kutoka Morocco, Noussair Mazraoui wamebakia kuwa nguzo muhimu pia.

Pia katikja safu ya ushambuliaji, winga Mbrazili David Neres -- aliyefunga katika mechi ya robo fainali dhidi ya Juventus mwaka 2019-- pia ni sehemu ya timu hiyo iliyo chini ya Ten Hag.

 

- sura mpya -

Ajax imewekeza baadhi ya fedha ilizopata kutokana na mauzo ya wachezaji wake katika kipindi cha miezi 18, ikitoa zaidi ya euro 15 milioni kumnunua mshambuliaji wa kimataifa wa Udachi, Quincy Promes kutoka Sevilla, kiungo wa Mexico, Edson Alvarez na mshambuliaji kijana Mbrazili, Antony.

Antony alitokea benchi na kufunga bao mwishoni mwa wiki. Pia aliyepachika bao mwingine katika mechi hiyo ni Mohammed Kudus, mchezaji wa kimataia wa Ghana mwenye umri wa miaka 20 aliyesajiliwa kutoka Nordsjaelland ya Denmark.

Ajax imeendelea kuamini vijana, lakini pia imeingiza wazoefu. Kiungo Davy Klaassen alinunuliwa kutoka Werder Bremen ya Ujerumani kwa euro 14 milioni na anarejea katika klabu aliyoiacha mwaka 2017 kwsenda Everton lakini akashindwa kung'ara.