Alat yaonya matangazo uchaguzi Serikali za mitaa

Muktasari:

  • Viongozi wa serikali za vijiji, mitaa na vitongoji wameonywa kuhusu matangazo yanayohamasisha uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwamba baadhi yanapotosha.

Dodoma. Viongozi wa serikali za vijiji, mitaa na vitongoji wameonywa kuhusu matangazo yanayohamasisha uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwamba baadhi yanapotosha.

Onyo hilo limetolewa leo Ijumaa Oktoba 11, 2019 jijini Dodoma na Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat), Elirehemu Kaaya.

Amesema maeneo mengi wamekuwa wakitangaza  kuhamasisha uandikishaji lakini wanakosea kufikisha ujumbe.

Kaaya amesema baadhi ya wanaotangaza hawaelezi kuhusu maana halisi ya kujiandikisha  badala yake wanazungumza wanayoyajua wao.

“Mamlaka wawaandikie matangazo ili wawe wanayasoma kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa,” amesema.

Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika Novemba 24, 2019.