Anayedaiwa kumnyanyasa mtoto wa miaka saba akutwa na kesi ya kujibu

Wednesday October 23 2019

 

By Pamela Chilongola, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na kesi ya kujibu Liziki Kessy, mkazi wa Kimara anayedaiwa kumnyanyasa mtoto wa miaka saba.

Mtuhumiwa huyo anayedaiwa kumwekea mtoto huyo uume mdomoni, kwenye haja kubwa na kumlisha kinyesi ataanza kujitetea Novemba 14, 2019.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Hudi Hudi ametoa uamuzi huo leo Jumatano Oktoba 23, 2019  baada ya wakili wa Serikali, Hilda Kato kuieleza mahakama hiyo kwamba imefunga ushahidi wake.

Hakimu Simba amesema mahakama hiyo imepitia vielelezo na ushahidi wa mashahidi watano wa Serikali,  kuonyesha kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 24, 2018 eneo la Kimara Stop Over, jijini Dae es Salaam.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 14, 2019.

Advertisement

Advertisement