Anayetuhumiwa kumuua mfanyakazi wake afikishwa mahakamani

Thursday March 26 2020

 

By Husna Issa, Mwananchi [email protected]

Arusha. Mamia ya watu wamejitokea leo Alhamisi Machi 26, 2020  katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kusikiliza kesi  inayomkabili Mkami Shirima (30) anayetuhumiwa kumuua mfanyakazi wake wa ndani,  Salome Zakaria(18) Machi 16, 2020.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakama akiwa kwenye ulinzi mkali huku akiwa amefunikwa sehemu kubwa ya mwili wake.

Akisoma mashtaka yanayomkabili, wakili wa Serikali Penina Joachimu amesema alifanya mauaji hayo eneo la Mianzini jijini Arusha na kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika  na kuomba mahakama  kupanga siku  nyingine ya kutajwa shauri hilo.

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi amesema  kesi hiyo itatajwa tena Aprili 8, 2020 na mshtakiwa kurudishwa mahabusu.

Mshtakiwa huyo pia amesomewa kesi ya nyingine ya usafirishaji wa dawa za kulevya  aina ya mirungi pamoja na Elias Lairien  .

Advertisement

Hakimu mkazi wa  Arusha Gwantwa Mwankuga ameahirisha a kesi hiyo hadi Aprili 8, 2020 kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Kesi hiyo ya kukutwa na mirungi ilitajwa kwa mara ya kwanza Septemba 24, 2019.

Advertisement