Apandishwa kizimbani kwa madai ya uhujumu uchumi, wizi wa chumvi

Tuesday October 22 2019

Mtuhumiwa Mohamedi Alikhan anaetuhumiwa kwa

Mtuhumiwa Mohamedi Alikhan anaetuhumiwa kwa mashtaka ya uchakachuaji fedha akiingia kwenye chumba cha mahabusu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Picha na Omar Fungo 

By Tausi Ally, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Meneja wa tawi la kampuni ya Neelkani Salt Limited, Mohammed Alikhan amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Katika Kesi hiyo namba 114 ya mwaka 2019, Alikhan anakabiliwa na mashtaka mawili ya utakatishaji  fedha na wizi wa katoni  45,919 za chumvi zenye thamani ya Sh413.5 milioni.

Akimsomea mashtaka leo Jumanne Oktoba 22, 2019 wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega amesema Alikhan  alitenda makosa hayo kati ya Januari Mosi,2018 na Julai 29, 2019.

Wakili Simon amedai kati ya siku hizo mtaa wa Arusha Ilala,  Alikhan akiwa meneja wa tawi la kampuni hiyo aliiba katoni hizo za chumvi aina ya Neel mali ya mwajiri wake zenye thamani ya Sh412.8 milioni.

Amedai mshtakiwa huyo pia katika kipindi hicho aliiba chumvi aina ya Neel Gold zenye thamani ya Sh720,000.

Wakili Simon amedai katika kipindi hicho mshtakiwa alitakatisha  Sh 413.5 milioni wakati akijiua fedha hizo zimetokana  na zao la makosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na wizi akiwa mwajiliwa.

Advertisement

Baada ya kusomewa mashtaka hayo hakuruhusiwa kuzungumza  chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na mshtakiwa kupelekwa rumande. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 5, 2019.

Advertisement