Askari aliyembaka mtoto wa askari mwenzake afukuzwa kazi

Muktasari:

Askari huyo wa usalama barabarani atapandishwa kizimbani leo mkuoni Kilimanjaro kutokana na tukio hilo

Moshi. Askari wa kikosi cha usalama barabarani, Willium Mwakatage anayedaiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba, ambaye ni mtoto wa askari mwenzake amefukuzwa kazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema taratibu za kijeshi zimekamilika ikiwa ni pamoja na kumfukuza kazi.

Kamanda Hamduni amesema baada ya taratibu hizo kukamilika wanatarajia kumpandisha mahakamani leo Ijumaa Februari 28, 2020.

Mwakatage alikamatwa na polisi wa mkoa hapa Februari 15, 2020 ikiwa ni baada ya kupita zaidi ya siku 40

bila kuonekana kituo chake cha kazi, baada ya kusambaa kwa taarifa za tukio hilo.