Benki kuu ya Tanzania yataja mambo 10 kunusuru mali za wakopaji kutouzwa

Muktasari:

Benki Kuu Tanzania (BoT) imekutana na wadau mbalimbali na kuwaelimisha maeneo 10 yatakayoondoa kero zinazosababisha dhamana za wateja kuuzwa kinyume na utaratibu.

Mbeya. Benki Kuu Tanzania (BoT) imekutana na wadau mbalimbali na kuwaelimisha maeneo 10 yatakayoondoa kero zinazosababisha dhamana za wateja kuuzwa kinyume na utaratibu.

Suluhu ya changamoto hizo zilizodumu kwa muda mrefu, BoT imesema imo kwenye utekelezaji wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 inayotoa ulinzi kwa wateja wa taasisi ndogo za fedha.

Mkurugenzi wa BoT tawi la Mbeya, Ibrahim Malogoi amesema wamebaini maeneo hayo 10 yanayotoa masharti magumu hivyo kusababisha wateja wengi kufilisiwa mali zao wanaposhindwa kufanya marejesho ya mikopo waliyochukua.

Miongoni mwa mambo yanayochangiwa kufilisiwa kwa wateja wa taasisi hizo, Malogoi alisema ni pamoja na kukopesha kwa vigezo na masharti magumu yanayosababisha madhara kwa wakopaji kiasi cha mali zao kuuzwa.

“Wateja wanatozwa riba na gharama kubwa za mkopo, hakuna uwazi wa masharti ya mikataba ya mikopo na kuna masharti magumu ya kulipa mikopo husika,” alisema Malogoi.

 

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumamosi Novemba 2, 2019