TANZIA: Baba wa Kanumba afariki

Muktasari:

Charles Kanumba ambaye ni baba wa marehemu Steven Kanumba amefariki akiwa anapatiwa natibabu.

Dar es Saalam. Baba wa marehemu Steven Kanumba amefariki dunia leo Jumapili ya March 8,2020 akipata matibabu katika Hospitali ya rufaa mkoa wa shinyanga.
Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa  na mtoto wake Mjanael Kanumba, alipozungumza leo Jumapili March 8, 2020 na Mwananchi.
Mjanaeli amesema baba yake amefariki leo saa nne asubuhi akiwa Hospitali ya rufaa mkoa shinyanga alipokuwa anapatiwa matibabu.

Mzee Kanumba kwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la nyonga lililosambabishwa kushindwa kutembea kwa muda mrefu na uvimbe katika kibofu cha mkojo pamoja na shinikizo la damu.
Amesema msiba upo nyumbani kwa baba huyo  Ngokolo mkoani Shinyanga na utaratibu wa ratiba za mazishi bado zinaelendea.