BancABC yatoa mkono wa pole kwa mteja wake

Wednesday September 4 2019

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Benki ya BancABC kampuni tanzu ya Atlas Mara Tanzania imetoa mkono wa pole wa Sh500,000 kwa Maria Privatus alifiwa na mume wake hivi karibuni.

Mbali na kutoa mkono wa pole huo, Benki ya BancABC pia imemfutia deni marehemu mumewe aliyekuwa mteja wa mkopo Rahisi ni moja ya huduma ambayo hutolewa na BancABC kwa ajili ya kufariji familia ya mteja wake inapotokea kifo kwa kufuta mkopo uliokuwa umebaki pamoja na kutoa msaada wa Sh500,000 kwa familia.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hiyo kwa Maria Privatus aliyefiwa na mumewe ambaye enzi za uhai wake alikuwa mteja wa BancABC wa mkopo Rahisi, Meneja wa benki hiyo kanda ya Dar es Salaam,  Ferdinand Mgeni alisema wana utaratibu wa kuipa mkono wa pole familia ambayo marehemu alikuwa mteja wa mkopo Rahisi.

"Tuliamua kuwa na kipengele cha aina hii kwenye huduma yetu ya Mkopo Rahisi ili tuwe tofauti na wengine kwenye soko.”

"Kikubwa ni kuipa faraja familia kwani mbali na kutoa rambi rambi ya Sh 500,000 pia tunafuta deni la mkopo ambao marehemu alikuwa anadaiwa," alisema.

Alifafanua kwamba, Mkopo Rahisi una riba ya chini kwa mwezi na unalenga kupunguza mzigo kwa wateja wakati wa kulipa ambao unaweza kuwa ndani ya miezi 72.

Advertisement

Akizungumzia faraja ya benki hiyo, Maria alisema hakutarajia faraja hiyo hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho ameondokewa na mwenzi wake.

"Pesa hii nitaiongeza katika mtaji wangu wa biashara ya chakula ninayofanya kwenye shule aliyokuwa akifundisha mume wangu, nitapambana ili nikuze mtaji ili niweze kuendesha familia kwani sasa mimi ndiye baba na mama wa familia," alisema.

Alisema atakuwa balozi mzuri wa BancABC kwani hakuwahi kuamini kama benki hiyo inaweza kufanya jambo hilo hadi ilipomtokea yeye ambapo licha ya kuwa katika kipindi kigumu, benki hiyo imemfanya asimame tena katika kipindi ambacho alikuwa katika wakati mgumu wa kuondokewa na mumewe.


Advertisement