Bavicha kutumia siku wa wapendanao kuhamasisha uandikishaji daftari la wapiga kura

Thursday February 13 2020

 

By Fortune Francis, Mwananchi [email protected]

Dar es salama. Baraza la vijana Chadema (Bavicha) limewataka watu wa kada mbalimbali kuitumia siku ya wapendanao kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Shughuli ya uboreshaji la daftari la wapiga kura  Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani linatarajia kufanyika kwa siku saba  kuanzia Februari 14 hadi 20, 2020.

Akizungumza leo Alhamisi Februari 13, 2020 Mwenyekiti wa Bavicha, John Pambalu amesema baraza hilo litatumia siku hiyo kuonyesha upendo kwa kuwahamasisha watu kwenda kujiandikisha.

"Sisi chadema tutatumia siku ya wapendanao kupita kila mahali kuhamasisha watu kwenda kujiandikisha iwe kwenye vijiwe, majumbani, ofisini tutawafikia wananchi wote.”

"Uwe mwana Chadema au wa chama chochote na hata kama huna chama tutakuomba ukajiandikishe na kutumia siku hiyo  kuhamasisha wengine kwenda kujiandikisha ,” amesema.

 

Advertisement

Advertisement