Benki ya Dunia yaipa Tanzania mkopo wa Sh1tri

Dar es Salaam. Benki ya Dunia (WB) imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola 450 za Marekani (Sh1.035 trilioni) kwa ajili ya mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) awamu ya tatu.

Katibu mkuu Wizara ya Fedha, Dotto James alisema tofauti na kipindi cha kwanza msisitizo wa kipindi cha pili ni kuimarisha uwezo wa walengwa kufanya kazi kwa kuwezesha kaya masikini.