Benki ya Dunia yakosoa punguzo bajeti ya elimu Tanzania

Thursday October 17 2019

By Elias Msuya, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Benki ya Dunia (WB) imesema licha ya Tanzania kuongeza uandikishaji wa wanafunzi wa shule za msingi, bajeti ya elimu imezidi kupunguzwa.

Akitoa matokeo ya utafiti leo Alhamisi Oktoba 17, 2019  jijini Dar es Salaam, mtaalamu wa elimu wa benki hiyo, Gemma Todd amesema bajeti kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019/20 ya elimu imeshuka kutoka asilimia 19 hadi 16.

"Ruzuku ya mwanafunzi imeshuka kutoka Sh336,891 hadi Sh220,566," amesema Todd.

Kuhusu ubora wa elimu, Todd amesema kutokana na ongezeko la wanafunzi, uwiano kati ya mwalimu na wanafunzi ni 1:82 huku kukiwa na mazingira magumu ya kufundishia.

"Wasichana na wanafunzi wenye umri mkubwa ndio wanaoathirika. Watoto milioni tatu walio chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa, jambo linalowaathiri kihisia na kimatendo," amesema.

Hata hivyo, amesema kumekuwa na ongezeko la wanafunzi kwa asilimia 19 tangu mwaka 2015/16.

Advertisement

"Watoto wanaojiunga na shule kwa umri sahihi wanaongezeka kwa asilimia 95. Wasiokuwepo shuleni ni asilimia 6.

Wengi wanaomaliza darasa la saba wanafaulu mtihani ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.8," amesema.


Advertisement