Bima ni kabla ya kuugua ili kupunguza gharama

Monday December 2 2019

By Julius Mnganga, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini Tanzania Bernard Konga amesema siku 30 zinazotolewa kabla mwanachama hajaanza kuitumia kadi yake.

Konga amesema endapo bima inayotolewa itatumika muda mfupi baada ya kutolewa, upo uwezekano wa wagonjwa kudanganya.

"Mtu anaweza akamwacha mgonjwa hospitalini na kwenda kukata bima aje kulipia gharama zake," amesema Konga.

Konga amesema hayo leo Jumatatu, Desemba 02, 2019 alipokuwa anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini Tanzania kuhusu mkakati wa mfuko huo kuboresha afya za wananchi na kufafanua kuhusu utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema matibabu hugharimu fedha nyingi hivyo umakini mwingi unahitajika kuhakikisha hakuna fedha ya ziada inatumika bila sababu za msingi.

Ingawa magonjwa yasiyoambukiza ndiyo hutumia kiasi kikubwa cha fedha za mfuko huo, takwimu zinaonyesha malaria, maambukizi ya njia ya mkojo pamoja na amoeba na magonjwa mengine ya tumbo ndio yanayoongoza kuugharimu mfuko huo.

Advertisement

Hata hivyo, mkurugenzi wa huduma za wanachama wa mfuko huo, Christopher Mapunda amesema mgonjwa mmoja wa saratani anahitaji zaidi ya Sh69.98 milioni wakati kusafisha figo ni Sh35.8 milioni wakati upasuaji mkubwa wa moyo akitumia Sh12.52 milioni kwa mwaka.

Advertisement