VIDEO: Bosi TCAA aeleza mchakato ufungaji wa rada

Muktasari:

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCCA), Hamza Johari ameeleza namna utekelezaji wa mradi wa rada mbili za kuongoza ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na ule wa Kilimanjaro (Kia)

Dar es Salaam. Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCCA), Hamza Johari ameeleza namna utekelezaji wa mradi wa rada mbili za kuongoza ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na ule wa Kilimanjaro (Kia).

Amesema eneo la kwanza ni shughuli zilizofanyika Ufaransa na Uingereza zikihusisha uundaji mitambo, majaribio ya kiwandani na kusafirisha mitambo kuja nchini.

Amesema shughuli nyingine ni mafunzo kwa wahandisi  na waongozaji ndege walioyapata nchini Ufaransa na Chuo cha kuongezea Ndege cha Afrika ya Kusini huku wataalamu 53 wakipata mafunzo hayo kati yao 12 wakipata mafunzo ya ukufunzi.

Johari ametoa maelezo hayo leo Jumatatu Septemba 16, 2019 mbele ya Rais John Magufuli katika hafla ya uzinduzi wa rada uwanjani hapo.

Amesema shughuli zilizofanyika nchini ni ujenzi wa majengo katika kituo cha Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro na usimikaji wa mitambo kwenye vyumba vya kuongezea ndege ambao umeshakamilika.

“Mradi huu ulihusisha kuunganisha mfumo unaoanisha mifumo mingine ya kusimamia anga iliyopo sanjari na mfumo wa ukokotoaji wa ankara,” amesema Johari.