CCM Karatu yarejesha halmashauri baada ya miaka 20

Arusha. Wagombea wa udiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) katika Kata tisa kati ya 12 ambazo kura zimemaliza kuhesabiwa wametangazwa kushinda.

Akizungumza na mwandishi msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Moris Waziri amesema sasa wanasubiri matokeo ya kata tatu tu ambazo wanakamilisha kuhesabu.

Amesema kata ambazo wanakamilisha kuhesabu ni pamoja na Karatu mjini na muda si mrefu watakamilisha.

Waziri amesema madiwani wawili katika jimbo hilo wa CCM walipita bila kupingwa.

 “Tunaendelea kuhesabu kura za ubunge yakikamilika tutatangaza matokeo,” amesema.