CCM yashinda jimbo la Handeni

Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la  Handeni,  Reuben Kwagilwa

Muktasari:

  • Katika matokeo hayo mgombea  wa ADC Twaha Said amepata kura 310, James Stima   wa Chadema kura 296 na Makame Semndili wa TLP akipata kura 31.

Handeni. Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la  Handeni,  Reuben Kwagilwa ametangazwa kushinda nafasi hiyo kwa kupata kura 15,241 huku aliyemfuatia mgombea wa CUF, Sonia Magogo akipata kura 6713.

Akitangaza matokeo hayo leo Alahamis Oktoba 29, 2020, msimamizi wa uchaguzi jimbo la Handeni mjini, Thomas Mzinga amesema ushindi wa mgombea ni wa asilimia 67 dhidi ya wagombea wote.

Katika matokeo hayo mgombea  wa ADC Twaha Said amepata kura 310, James Stima   wa Chadema kura 296 na Makame Semndili wa TLP akipata kura 31.

Aidha, katika uchaguzi huo, kata 12 za halmashauri ya mji zote wamepita Madiwani wa CCM.